GONZI RAI AITAKA SERIKALI KUDHIBITI KERO LA NDOVU KINANGO

Mbunge wa Kinango, Idd Gonzi Rai, ameitaka serikali kuchukua hatua za haraka kukabiliana na kero la ndovu katika wadi za Ndavaya, Puma, Samburu Chengoni na Mackinnon, akisema hali hiyo imekuwa changamoto ya muda mrefu kwa wakazi wa maeneo hayo.
Akizungumza katika wadi ya Mackinnon, Rai amesema uvamizi wa ndovu umekuwa ukiwatia hofu wakazi, huku ukiathiri shughuli za kiuchumi na juhudi za maendeleo katika maeneo yanayokumbwa na tatizo hilo.
Mbunge huyo amesema wakulima wamekuwa wakipata hasara kutokana na ndovu kuvamia mashamba na kuharibu mazao, hali inayoweza kuathiri usalama wa chakula na mapato ya familia zinazotegemea kilimo kujikimu.
Rai ameitaka idara inayohusika na usimamizi wa wanyamapori kuweka uzio na kutekeleza mikakati mingine ya kudhibiti mienendo ya ndovu, akisisitiza umuhimu wa kulinda maisha ya wananchi na mali zao.
Amesema hatua madhubuti zinahitajika ili kupunguza migogoro kati ya binadamu na wanyamapori na kuwawezesha wakazi kuendesha shughuli zao za kila siku bila hofu ya uvamizi wa ndovu.
Kero la ndovu limeendelea kuwa changamoto katika maeneo ambako makazi ya binadamu na shughuli za kilimo zinakutana na maeneo ya wanyamapori. Mikakati ya kudhibiti uvamizi huo ni muhimu katika kulinda maisha ya wananchi, mazao na mifugo, huku pia ikizingatia uhifadhi wa wanyamapori.
