Video Muhimu
Kombo Ataka KWS Kudhibiti Ndovu Wanaovamia Makazi
Naibu Gavana Chirema Kombo ameitaka Idara ya Huduma kwa Wanyamapori nchini (KWS) kuchukua hatua za haraka kudhibiti ndovu wanaovamia makazi na mashamba ya wakazi, kufuatia kujeruhiwa vibaya kwa mwalimu mmoja wa Shule ya Msingi ya Egu. Kombo amesema uvamizi wa ndovu katika maeneo ya makazi unahatarisha maisha ya wananchi na kuathiri shughuli zao za kila siku, huku wakazi wakikabiliwa na hofu ya kushambuliwa na wanyamapori hao. Ametaka KWS kuimarisha mikakati ya kudhibiti wanyamapori na kuhakikisha usalama wa wananchi unazingatiwa ili kuzuia visa zaidi vya majeraha na uharibifu wa mali. Tukio hilo limeibua tena wasiwasi kuhusu mzozo kati ya binadamu na wanyamapori, hasa katika maeneo ambayo ndovu huvamia mashamba na makazi ya watu.
Credits: Shem OburuVICTOR NYANJE AWATAKA WAKAZI WA KWALE KUMUUNGA MKONO RAIS RUTO KWA ASILIMIA 100
Mwakilishi wa Wadi ya Kasemeni, Victor Safari Nyanje, ameitaka jamii, hususan wakazi wa Kaunti ya Kwale, kumuunga mkono Rais William Ruto kwa asilimia 100, akisema kuwa kwa mara ya kwanza chini ya uongozi wa Rais huyo, eneo hilo limetambuliwa katika ngazi ya kitaifa. Nyanje amesema hatua hiyo ni ishara ya maendeleo na kutambuliwa kwa wananchi wa eneo hilo, hivyo akawataka kuendelea kumuunga mkono Rais Ruto ili kuhakikisha mafanikio zaidi yanapatikana kwa manufaa ya jamii.
Credits: Patrick MangaleLunganzi Chai Mangale Awataka Wakazi wa Kwale Kukataa Viongozi Wanaohusishwa na Ufisadi
Mwaniaji wa ugavana wa Kwale, Lunganzi Chai Mangale, amewataka wananchi kukataa viongozi wanaotumia vibaya mamlaka ya umma kujinufaisha binafsi. Akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mashujaa katika eneo la Mpirani, Kasemeni, amesema uongozi bora hupimwa kwa uadilifu, uwajibikaji na huduma kwa wananchi. Mangale pia amemtaja Rais William Ruto kuwa shujaa kwa vitendo na kuonya kuwa ufisadi na ubadhirifu wa fedha za umma hudhoofisha maendeleo na utoaji wa huduma muhimu.
Credits: Patrick MangaleMBUNGE WA LUNGALUNGA ATISHIA KUUNGANA NA WANANCHI KUKABILIANA NA NDOVU
Mbunge wa Lungalunga, Mangale Chiforomodo, ametishia kuungana na wananchi wa eneo hilo kukabiliana na ndovu iwapo shirika linalohusika na uhifadhi wa wanyamapori litashindwa kuchukua hatua kukomesha kero zinazowakabili wakazi hao
Credits: Patrick MangaleLunganzi Mangale Amtetea Ruto Kuhusu Ugavi wa Mashamba Kwale
Mhandisi na mwaniaji wa kiti cha ugavana wa Kaunti ya Kwale, Lunganzi Chai Mangale, amemtetea Rais William Ruto dhidi ya lawama zinazohusishwa na masuala ya ugavi wa mashamba, akisema kuwa wakazi wa Lunga Lunga wanapaswa kuelekeza malalamishi yao kwa Serikali ya Kaunti ya Kwale.
Credits: Patrick MangaleVijana Diani Waandamana Kudai Uchunguzi wa Haraka wa Kifo cha Hassan
Baadhi ya Vijana Diani waandaamana kushinikiza serikali kuharakisha uchungunzi wa marehemu Hassan ambaye alifariki katika mazingira tatanishi akiwa amefungwa miguu na mikono kwa kamba na kutupwa katika barabara ya cabros ya Bahari Dhow . Wakisema wanataka majibu kuhusu kulichopelekea kifo cha mwenzao.
Credits: Shem OburuSteve Ruwa Mwanza Atangaza Kugombea Useneta Kwale kwa Tiketi ya UDA 2027
Mfanyibiashara kutoka Dzivani wadi ya Kinango kaunti ya Kwale Steve Ruwa Mwanza ametangaza azma yake ya kugombea kiti cha Useneta wa Kwale mwaka 2027 kwa tiketi ya UDA. Mwanza amesema anaunga mkono serikali ya Rais William Ruto, akisema Rais Ruto anaendelea kushirikiana a viongozi kutoka matabaka mbalimbali.
Tesla Inafichua Roadster Inayoweza Kuruka kwa Teknolojia ya Roketi ya SpaceX
Tesla imefichua Roadster yake ya kizazi kipya ikijumuisha vichocheo vya mtindo wa roketi vilivyotengenezwa na SpaceX. Gari la umeme la michezo lilifanya manevu ya anga wakati wa onyesho la tarehe 15 Oktoba, na uzalishaji unatarajiwa kufanyika mwaka 2028.
Credits: Joe Sudi- SB Extra (Tiktok) & abc news (Youtube)Oburu Odinga anazima uvumi wa afya, anasema yuko sawa
Oburu Odinga anazima uvumi kuhusu afya yake, akawaambia Wakenya kwamba amekuwa mgonjwa, kama kila Mkenya mwingine, lakini sasa yuko sawa. Anawapa umma hakikisho kuhusu hali yake katikati ya wasiwasi unaoongezeka kuhusu afya yake.
Credits: Shem OburuWanne wamejeruhiwa jengo la zamani la Club Avenida likianguka wakati wa uharibifu katika CBD ya Nairobi
Watu wanne wamejeruhiwa baada ya jengo ambalo lilikuwa na Club Avenida kuanguka wakati wa uharibifu kando ya Barabara ya Moi katika CBD ya Nairobi. Maafisa wa Kaunti ya Nairobi wameomba uchunguzi wa sababu ya kuanguka na ufuatiliaji wa kanuni za usalama.
Credits: Joe sudi- Tiktok: Mambo ni liveWAFUATAO 4 WAMEKUFU, 16 WAMEJIDUNDUA KATIKA AJALI YA BARABARA KWA MERU
Watu wanne, wanaume watatu na mwanamke mmoja, wamekufa wakati wengine 16 walipata majeraha baada ya lori kuripotiwa kuondoka barabarani na kugonga magari kadhaa na wafanyabiashara wa kando ya barabara katika Riverland, jiji la Meru.
MATOKEO YA MOTOKO KATIKA BUNGANO LA KAUNTI YA KWALE
Moto ulijitokeza katika jengo la umeme wa jua la Bunge la Kaunti ya Kwale, likalazimisha wafanyakazi na watu wa karibu kutoroka kwa usalama na kusababisha woga katika eneo lililoko karibu na mahakama za mtaa na ofisi za kampuni ya maji.
Credits: Alloys MusyokaBandari ya Lamu inapokea meli inayobeba vifaa kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda cha mafuta
Meli inayobeba vifaa kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda cha mafuta imefika Bandari ya Lamu kutoka China. Usafirishaji huu unaashiria hatua nyingine katika maendeleo ya mradi wa kiwanda cha mafuta, ambapo vifaa vinatarajiwa kusaidia kazi za ujenzi na usakinishaji zinazoendelea katika kituo hicho. Tazama video ili kuona meli na vifaa vilivyolekezwa Bandari ya Lamu.
Credits: By reporter from lamu.