Pwani Yetu News Logo

PWANI YETU
NEWS

CRIME

MLINZI WA KAMPUNI YA ULINZI AJERUHIWA VIBAYA KATIKA SHAMBULIO LA GENDE LA WATU WENYE MAPANGA LIKONI

Imechapishwa 3 Nov 2026 saa 7:03 AM
1 dakika za kusoma
MLINZI WA KAMPUNI YA ULINZI AJERUHIWA VIBAYA KATIKA SHAMBULIO LA GENDE LA WATU WENYE MAPANGA LIKONI

Mfanyakazi wa kampuni ya ulinzi ya kibinafsi amejeruhiwa vibaya baada ya kushambuliwa na kundi la vijana waliokuwa wamejihami kwa mapanga katika eneo la Likoni, Kaunti ya Mombasa.

Kelvin Mwangi Mbuthia, mwenye umri wa miaka 30, ambaye ni mfanyakazi wa kampuni ya Sarman Security, anadaiwa kushambuliwa alfajiri ya leo alipokuwa akielekea kazini kupitia kivuko cha Likoni.

Kwa mujibu wa Mwangi, tukio hilo lilitokea majira ya saa 11:30 alfajiri katika eneo la Patana, karibu na Hospitali ya Wilaya ya Likoni, alipokutana na kundi la takriban vijana kumi waliokuwa wamejihami kwa mapanga.

Anasema vijana hao walimvamia na kumpiga kabla ya kutoroka na simu yake aina ya Tecno Spark 50.

Mwangi alipata majeraha makubwa kichwani na kusaidiwa na wasamaria wema waliomkimbiza katika Hospitali ya Wilaya ya Likoni kwa matibabu. Baada ya kupatiwa huduma ya kwanza na matibabu, aliruhusiwa kurejea nyumbani.

Tukio hilo limeripotiwa katika Kituo cha Polisi cha Likoni chini ya nambari ya OB 02/02/11/2026.

Shambulio hilo linajiri wiki chache baada ya matukio mengine ya vurugu kuripotiwa katika maeneo ya Shikaadabu na Barabara ya Dongo Kundu, ambapo watu wawili waliripotiwa kuuawa huku wengine wawili wakijeruhiwa.

Matukio hayo yanaibua wasiwasi kuhusu usalama wa wakazi wa Likoni, hasa wanaosafiri nyakati za alfajiri na usiku.

Pata habari muhimu moja kwa moja kwenye Email yako

Jiunge na maelfu ya wasomaji wa Pwani Yetu News.

MLINZI AJERUHIWA VIBAYA KATIKA SHAMBULIO LA MAPANGA LIKONI | Pwani Yetu News