Pwani Yetu News Logo

PWANI YETU
NEWS

CRIME

MWANAUME AHUKUMIWA MAISHS KWA KUMNAJISI MTOTO KWALE

Imechapishwa 23 Okt 2026 saa 11:06 AM
1 dakika za kusoma
MWANAUME AHUKUMIWA MAISHS KWA KUMNAJISI MTOTO KWALE

Mwanaume mwenye umri wa miaka 25, Athmani Juma, amehukumiwa kifungo cha maisha gerezani baada ya kupatikana na hatia ya kumnajisi mtoto wa miaka saba katika kijiji cha Vilalani, Kaunti ya Kwale.

Hukumu hiyo ilitolewa na Hakimu Leah Wandia Kabaria katika Mahakama ya Msambweni, kufuatia ushahidi uliowasilishwa wakati wa kusikilizwa kwa kesi hiyo.

Mahakama ilibaini kuwa kosa hilo lilitendeka Juni 7, 2025, ambapo mshtakiwa alimpata mtoto huyo na kumwingilia kinyume na maumbile.

Kesi hiyo inasisitiza umuhimu wa kulinda watoto dhidi ya ukatili wa kingono na kuwawajibisha wahalifu kwa mujibu wa sheria.

Pata habari muhimu moja kwa moja kwenye Email yako

Jiunge na maelfu ya wasomaji wa Pwani Yetu News.

MWANAUME AHUKUMIWA MAISHS KWA KUMNAJISI MTOTO KWALE | Pwani Yetu News