Pwani Yetu News Logo

PWANI YETU
NEWS

Pwani

POLISI WAMKAMATA MSHUKIWA WA WIZI WA PIKIPIKI KWALE

Imechapishwa 14 Okt 2026 saa 6:38 PM
1 dakika za kusoma
POLISI WAMKAMATA MSHUKIWA WA WIZI WA PIKIPIKI KWALE

Polisi wamemkamata mshukiwa mmoja wa wizi wa pikipiki katika eneo la Mwabungo, kaunti ya Kwale, na kurejesha pikipiki iliyoibwa katika eneo la Neptune, Diani.


Kwa mujibu wa ripoti ya polisi, pikipiki hiyo ilikuwa tayari imetenganishwa vipande na kufichwa kwenye dari ya nyumba moja katika eneo la Mwabungo ilipopatikana.

Pikipiki hiyo aina ya Haojin Hawk, yenye nambari ya usajili KMFJ 189K, ilikuwa imeibwa katika eneo la maegesho.

Article imageMshukiwa, Mohammed Athuman Mwaruphia



Mshukiwa, Mohammed Athuman Mwaruphia, mwenye umri wa miaka 22, alikamatwa baada ya polisi kupata taarifa kutoka kwa wananchi zilizowaelekeza katika nyumba ambako pikipiki hiyo ilikuwa imefichwa.

Mshukiwa anazuiliwa katika kituo cha polisi cha Diani akisubiri kufikishwa mahakamani kuhusiana na wizi huo.

Pata habari muhimu moja kwa moja kwenye Email yako

Jiunge na maelfu ya wasomaji wa Pwani Yetu News.

POLISI WAMKAMATA MSHUKIWA WA WIZI WA PIKIPIKI KWALE | Pwani Yetu News