Pwani Yetu News Logo

PWANI YETU
NEWS

Siasa

LUNG’ANZI CHAI MANGALE AKUTANA NA SIMBA ARATI KUIMARISHA ODM KAUNTI YA KWALE

Imechapishwa 3 Nov 2026 saa 6:44 AM
1 dakika za kusoma
Lung’anzi Chai Mangale akiwa katika mkutano na Gavana wa Kisii Simba Arati kujadili uimarishaji wa chama cha ODM katika Kaunti ya Kwale.  8. Tags:

Mgombea wa kiti cha ugavana wa Kaunti ya Kwale, Lung’anzi Chai Mangale, amekutana na Naibu Kiongozi wa Chama cha Orange Democratic Movement (ODM) na Gavana wa Kaunti ya Kisii, Simba Arati, katika mazungumzo yaliyolenga kuimarisha chama hicho katika eneo la Pwani.

Mazungumzo hayo yalijikita katika mikakati ya kukijenga chama cha ODM kuanzia ngazi ya mashinani, kuimarisha ushirikiano miongoni mwa wanachama na kupanua ushawishi wake wa kisiasa katika Kaunti ya Kwale.

Viongozi hao pia walijadili namna ya kukiimarisha chama hicho na kukiweka katika nafasi nzuri kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2027.

Mkutano huo unaashiria juhudi za kuimarisha misingi ya ODM katika Kaunti ya Kwale huku maandalizi ya kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu ujao yakiendelea kushika kasi.

Pata habari muhimu moja kwa moja kwenye Email yako

Jiunge na maelfu ya wasomaji wa Pwani Yetu News.

LUNG’ANZI MANGALE NA SIMBA ARATI WAIMARISHA ODM KWALE | Pwani Yetu News