Pwani Yetu News Logo

PWANI YETU
NEWS

Habari za Taifa

WATOTO WANNE WA FAMILIA YA MDAVE WALIOFARIKI KATIKA AJALI YA MTITO ANDEI WAZIKWA KINANGO

Imechapishwa 4 Nov 2026 saa 9:27 PM
1 dakika za kusoma
Familia ya Spencer Mdave imewaaga watoto wake wanne waliofariki katika ajali ya basi la kanisa na lori eneo la Kanga, karibu na Mtito Andei.

Watoto wanne wa familia ya Spencer Mdave waliofariki katika ajali mbaya ya barabarani iliyotokea eneo la Kanga, karibu na Mtito Andei, wamezikwa leo katika hafla ya mazishi iliyofanyika nyumbani kwao Kinango, Kaunti ya Kwale.

Watoto hao waliotambuliwa kama Sarah Mdave, Sharon Mdave, Shekinah Mdave na Salem Mdave, walipoteza maisha mnamo Oktoba 25, 2026, katika ajali iliyohusisha basi la kanisa na lori.

Hafla hiyo ya mazishi imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa eneo hilo, akiwemo Naibu Gavana wa Kwale Chirema Kombo, Mbunge wa Kinango Gonzi Rai pamoja na wawakilishi wa wadi, ambao wameungana na familia, jamaa na wakazi wa Kinango kuwaaga watoto hao.

Kifo cha watoto hao wanne kutoka familia moja kimeiacha familia ya Spencer Mdave pamoja na jamii ya Kinango katika majonzi makubwa, huku wakazi wakishiriki kuifariji familia kufuatia msiba huo.

Ajali hiyo iliyotokea eneo la Kanga, karibu na Mtito Andei, ilisababisha vifo vya watu 24, wakiwemo watoto hao wanne, huku wengine kadhaa wakipata majeraha.

Pata habari muhimu moja kwa moja kwenye Email yako

Jiunge na maelfu ya wasomaji wa Pwani Yetu News.

WATOTO WANNE WA FAMILIA YA MDAVE WALIOFARIKI KATIKA AJALI YA MTITO ANDEI WAZIKWA KINANGO | Pwani Yetu News