Naibu Gavana Kombo Ataka KWS Kudhibiti Ndovu Wanaovamia Makazi

Naibu Gavana wa Kwale, Chirema Kombo, ameitaka Huduma ya Wanyamapori nchini (KWS) kuchukua hatua za haraka kudhibiti ndovu wanaovamia makazi na mashamba ya wakazi wa kaunti hiyo.
Akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mashujaa ya mwaka 2026 yaliyofanyika Lungalunga, Kombo alifichua kuwa mwalimu mmoja wa Shule ya Msingi ya Egu amejeruhiwa vibaya na ndovu.
Alitaka KWS kuhakikisha ndovu hao wanaondolewa katika maeneo ya makazi ndani ya wiki mbili, akisema wakazi wameendelea kukabiliwa na changamoto ambazo zinaweza kutatuliwa.

Kwa upande wake, Kamishna wa Kaunti ya Kwale, David Rotich, aliwahakikishia wakazi kuwa serikali itachukua hatua kukabiliana na ukosefu wa usalama na mzozo kati ya binadamu na wanyamapori.
Rotich alisema serikali inatambua kuwa ndovu wamekuwa wakiharibu masham
